Zana ya bure

Link na QR code ya WhatsApp, bure.

Tengeneza link na QR code zinazofungua chati na biashara yako, ujumbe wako ukiwa tayari umeandikwa. Kwa bio ya TikTok na Instagram, mabango na vipeperushi. Bure, bila kujisajili.

+254

Unaandikwa tayari kwa ajili yao; wanaweza kuubadilisha kabla ya kutuma.

Weka namba yako upate link na QR code yako.

Bure, bila kujisajili. Namba yako haitoki kwenye kivinjari chako.

QR code yako

Ichapishe kwenye mabango, vipeperushi, risiti na kaunta ya duka lako.

Chapisho gani lilileta mteja huyo?

Link za kampeni za SentePoint zinahesabu mibofyo, chati, oda na mauzo ya M-Pesa kutoka kila video ya TikTok, chapisho na bango. Kisha msaidizi wake wa AI anajibu chati hizo kwa ajili yako, mchana na usiku.

Jaribu SentePoint bure kwa siku 14

Jinsi ya kutengeneza link yako ya WhatsApp

  1. 1

    Weka namba yako

    Chagua nchi yako na uandike namba yako ya WhatsApp.

  2. 2

    Ongeza ujumbe

    Si lazima: maneno ambayo chati ya mteja wako itaanza nayo.

  3. 3

    Shiriki

    Nakili link kwa ajili ya bio na machapisho yako, au pakua QR code uichapishe.

Maswali

Link ya WhatsApp (link ya wa.me) ni nini?

Ni link inayofungua chati ya WhatsApp na namba yako, bila mteja kulazimika kuhifadhi namba yako kwanza. Unaweza pia kuwaandikia ujumbe tayari, kama “Habari! Ningependa kuagiza”. Inafanya kazi kwenye simu na WhatsApp Web.

Ninawekaje link ya WhatsApp kwenye bio ya TikTok au Instagram?

Nakili link yako, kisha kwenye TikTok nenda Edit profile → Website (TikTok inaweza kuhitaji akaunti ya biashara kuonyesha link kwenye bio), au kwenye Instagram nenda Edit profile → Links → Add external link. Kwenye video zako, sema “link iko kwenye bio” ili watu wajue kuibonyeza.

QR code ya WhatsApp naweza kuitumia wapi?

Ichapishe popote watu wanaposimama mbele ya biashara yako: mabango, vipeperushi, menyu, risiti, mifuko ya kuletea, kaunta ya duka au kibanda chako. Wakiiskani kwa kamera ya simu, chati na wewe inafunguka.

Inafanya kazi na namba ya WhatsApp Business?

Ndiyo. Link inafanya kazi kwa namba yoyote ya WhatsApp, ya kawaida au ya Business, ili mradi namba iko kwenye WhatsApp.

Ni bure kweli? Mnahifadhi namba yangu?

Ni bure na haihitaji kujisajili. Link na QR code zinatengenezwa kwenye kivinjari chako, na namba yako haitumwi kwetu wala kuhifadhiwa.

Nitajuaje chapisho au bango gani lilileta mteja?

Link ya kawaida ya WhatsApp haiwezi kukuambia. Link za kampeni za SentePoint zinampa kila video ya TikTok, chapisho au bango link yake, kisha zinahesabu mibofyo, chati, oda na mauzo ya M-Pesa kila moja inaleta, na msaidizi wake wa AI anajibu chati hizo kwa ajili yako.

Ongea nasi